Religion
Read books online » Religion » Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) by Susan Davis (ebook reader browser .TXT) 📖

Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) by Susan Davis (ebook reader browser .TXT) 📖». Author Susan Davis



1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 ... 17
Go to page:
KUHUSU UNABII HUU

Susan ana kipaji cha unabii. 1 Wakorintho 14:1 yasema “Ufuateni upendo na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.” Tunaishi na tunahitajika kutii maagizo ya Mungu katika Agano Jipya. Ijapo kuna baadhi wanao amini kuwa vipaji vya kiroho kama unabii havipo tena. La sivyo. Hizi ni fikra za ubinadamu wala sio za Mungu. Mungu hajabadili agano lake. Tungali katika enzi za Agano Jipya. Tafadhali nawaomba muelewe ya kwamba sharti lako la kwanza ni kwa Bwana Yesu Kristo na neno lake kama ilivyoandikwa kwenye Bibilia. Hasa Agano Jipya. Kama ipasavyo, unabii wote wafaa kupimwa kulingana na Bibilia. Ikiwa unabii unalingana na Bibilia, basi tunatarajiwa kutii. Kwa sasa, Mungu hatumii unabii ili kutuletea imani au kanuni mpya, bali anautumia ili kuimarisha maneno yake ambayo tayari ametupa katika Bibilia. Mungu pia anatumia unabii kutuonya binafsi kuhusu matukio yajayo ambayo yatatuathiri.

Jinsi ilivyo katika Agano la Kale, Mungu hutumia manabii katika nyakati hizi za Agano Jipya. Katika kitabu cha Matendo ya Mitume ambacho kimo kwenye Agano Jipya kinataja manabii kama Yuda na Sila (Matendo ya Mitume 15:32) na Agabo (Matendo ya Mitume 21:10) na wengine wengi. Huduma ya wanabii inazungumziwa pia katika 1 Wakorintho 12:28; 14:1, 29, 32, 37 na hali kadhalika katika Waefeso 2:20; 3:5; 4:11. Yesu huwachagua manabii wamtendee kazi duniani. Pia Yesu anatumia unabii na manabii kutueleza matakwa yake kwetu wanawe. Bibilia iliandikwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Kuna baadhi ya watu wanaosema kuwa unabii unaweza kuongezea ua kupunguza maandiko ya Bibilia. Bibilia yenyewe inasema kuwa unabii ni moja ya karama za Roho Mtakatifu. Bibilia inaongezewa au kupunguzwa wakati watu wanaongezea maneno yao wenyewe kupitia fafanuzi mbali mbali na hata kuongezea dhana zao wenyewe ambazo hazitoki kwa Mungu na zinatokana na mawazo ya kipagani. Kazi ya kimsingi ya wanabii katika Bibilia imekuwa na itaendelea kuwa ya kuwarejesha watu kwa neno la Mungu na kwa Bibilia kama inavyosema katika 1 Wathesalonika 5:19-21“Msimzimishe Roho; msitweze unabii; jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema.” Jinsi ya kujaribu ujumbe huu ni kwa kulinganisha yaliyomo na yale Bibilia isemayo. Katika unabii wote ulioko hapa, mimi binafsi (Mike Peralta) nimeujaribu ujumbe wote ulioko hapa na unakubaliana na Bibilia. Ningependa wewe msomaji pia ujaribu ujumbe huu mwenyewe na kuulinganisha na Bibilia. Ikiwa unalingana na Bibilia, basi ni dhahiri kuwa Mungu anakutaka uutwae kwenye moyo wako na kuyatii maagizo yake.

 

YALIYOMO

Utambulisho kutoka kwa Bwana Yesu

Sura ya 1. Unyenyekevu

Sura ya 2. Msiweke imani yenu kwenu wenyewe au kwa wengine

Sura ya 3. Jifunzeni unyenyekevu

Sura ya 4. Kumuamini Mungu

Sura ya 5. Msamaha

Sura ya 6. Ishini duniani ila msiwe mmoja wa “wale wa dunia”

Sura ya 7. Unyakuo na Karamu ya Arusi ya Mwana Kondoo

Sura ya 8. Jitayarisheni kwa unyakuo

Sura ya 9. Kuhusu Kanisa lililopotea

Sura ya 10. Tamaa ya ulimwengu

Sura ya 11. Ulimwengu unaelekea kwenye dhiki

Sura ya 12. Naja hivi karibuni

Sura ya 13. Muda unayoyoma wanangu

Sura ya 14. Ulimwengu umenigeuka

Sura ya 15. Wachungaji hawanifuati

Sura ya 16. Wakati wa kurudi kwangu umewadia

Sura ya 17. Kuhusu Mpinga Kristo

Sura ya 18. Wakati unakaribia wa kurudi kwangu

Sura ya 19. Jitayarisheni

Sura ya 20. Wakati wenu u karibu kwisha 

Sura ya 21. Mbali na mapenzi yangu mwanipinga

Sura ya 22. Uovu waja kuuteketeza ulimwengu

Sura ya 23. Saa sita ya usiku inakaribia

Sura ya 24. Acheni kupigana wenyewe kwa wenyewe

Sura ya 25. Sitawachukua ikiwa mngali na dhambi ambayo hamjatubu

Sura ya 26. Nitazameni mimi

Sura ya 27. Hamna budi kujitayarisha ikiwa mwataka kuja nami

Sura ya 28. Uzima wenu wa milele u mashakani

Sura ya 29. Lazima munikimbilie sasa sio kutembea

Sura ya 30. Bi arusi wangu apendeza kwa njia zake zote

Sura ya 31. Ni wachache sana wanaoniabudu na kutubu kwangu

Sura ya 32. Ni karibu kumuondoa bi arusi wangu na kumpelekea mahali palipo salama

Sura ya 33. Aidha mnipe nafasi ya kwanza ama msinipe nafasi yoyote ile

Sura ya 34. Kuna dhiki yaja – dhiki kuu

Sura ya Sura ya 35. Hakuna manufaa yoyote kuiikimbiza dunia inayokufa

Sura ya 36. Wengi wadhaniao wa tayari wajidanganya

Sura ya 37. Muda uliosalia ni mfupi sana

Sura ya 38. Wafuasi wangu kamili wanakesha wakiningojea - wanajiadhari

Sura ya 39. Ushuhuda

 

 

UTAMBULISHO KUTOKA KWA BWANA

 

Wanangu, huyu ni Bwana wenu anayenena nanyi. Naja kwa upesi. Kurudi kwangu kumewadia, Ni mlangoni. Naja! Jitayarisheni.

 

Ujumbe huu uliandikwa na binti yangu Susan akiwa kwa mfungo wa siku arobaini, kwa ombi langu. Nilimleta mahali faragha ili aweze kujinyima. Nilimpa maneno mengi niliyotaka yawajie ninyi wanangu. Kwa hivyo aliyaandika jinsi nilivyo mwelekeza. Barua hizi zote zina ujumbe maalum ambao mnahitajika kuusoma na kutafakari kwa maana kurudi kwangu kumekaribia.

 

Ni Mimi Bwana na Mwokozi wenu,

 

YAHUSHUA (Yesu Kristo) 

 

 

 

 

 

 

USHUHUDA

Maneno haya yote aliyasema Mungu Baba, na mwanawe YAHUSHUA HA MASHIACH (Yesu Kristo au Yesu Mwenye upako au Yesu Masiya) kwa Susan akiwa kwa mfungo wa siku arobaini. Maneno haya yalirekodia kati ya Januari 27, 2012 na Machi 6, 2012.

 

USHUHUDA

Nakushukuru sana kwa barua zako pepe unazotutumia ukituelezea maneno ya Mungu. Niliomba na kumuuliza Roho Mtakatifu aniongoze niweze kuelewa mambo mengi na kutembea kwa njia za Bwana. Niombee. Mungu aibariki huduma yako. – Msomaji wa 1

 

Dada Susan, asante sana YAHUSHUA kwa barua hizi na yote yale uliompitishia binti yako ili aziandike. Nilianza kuzisoma na ninasoma kurasa kumi kila siku. Nimebarikiwa. – Msomaji wa 2

Susan, asante sana kwa barua hizi. Zimenibariki sana na ninahisi moyo wangu ukiona njaa ya kumjua Bwana YAHUSHUA. –msomaji wa 3

 

Dadangu Susan, naelekea kumaliza kusoma barua hizi za Mungu. Kweli ni maneno ya ajabu. Nashindwa kuweka kitabu chini. Ukweli wake, hekima yake na jinsi anatusihi tumfuate ni ajabu. Ni mnyenyekevu na mwenye upendo anavyotuhimiza, na kuonya mataifa. Namshukuru kwa yote. Ubarikiwe sana. – Msomaji wa 4

 

Susan, asante sana dada kwa kunitumia barua hizi. Zimenifanya nimuabudu Mungu. Naomba mamilioni ya watu watafanya vivi hivi. Mungu akubariki sana kwa utiifu wako na uaminifu wako kwake. Upendo wa milele ndani ya Masiya. – Msomaji wa 5

 

Susan, huu ni unabii ulio na upako mkuu kutoka kwa Bwana. Nimesoma unabii mwingi tangu nilipokuwa mkristo mchanga mwaka wa 1979. Nimesikia na kusoma unabii mwingi kwa miaka 33 lakini maneno yaliyoko katika kitabu hiki ndiyo maneno yaliyo na upako mkuu niliyo yasikia maishani mwangu mwote.- Mike Peralta (aliyekiandika kitabu hiki)

 

SURA YA 1: UNYENYEKEVU

Unyenyekevu ni utufu. Ni kukubali kuwatumikia wengine bila manung’uniko, kuwasamehe wenzako wanapokukosea. Ni kuwa na hamu ya kuwatumikia wengine na kumpendeza Mungu. Ni kutaka kumtumikia Bwana kila wakati kwa matumaini. Ni kuwa na moyo ulio tayari kumtumikia Bwana na watu wengine. Unyenyekevu pia ni kukubali kuwa wa mwisho, usiyeonekana hadharani.

Luka Mtakatifu 14:7-11. Akawaambia mfano wale walioalikwa alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele, akasema, Ukialikwa na mtu harusini, usiketi katika kiti cha mbele isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kukuliko wewe, akaja Yule aliyewaalika wewe na yeye na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma. Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya watu wote walioketi pamoja nawe. Kwa maana kila ajikwezaye atadhaliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.

Mathayo Mtakatifu 19:30. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.

Ni yule mtu ambaye anasahaulika kwa maana yeye ni mtu duni, anachanganyika na mandhari. Hawataki kuwa katikati ya mambo. Wanataka wafichike mbali, polepole, wakimtii Mungu. Huu ndio unyenyekevu, binti yangu na huyu ndiye bi arusi wangu.

Yeye ni hivi vitu vyote nilivyotaja. Sasa wayaona makosa yako binti yangu? Tuendelee…

Kuwa mnyenyekevu maana yake ni nini? Ni kufanya kazi bila kuonekana na bila kutamani umaarufu. Ni kumtii Mungu kikamilifu. Ni kutafuta kumtii Mungu katika mambo yote. Unyenyekevu ni kutojali yale watu wengine wanafikiria juu yako. Ni kuwatendea wengine bila kusifiwa. Ni kutamani fadhili kutoka kwa Mungu wala sio kwa binadamu. Ni kukuwa katika fadhili za Mungu na kumpendeza Mungu.

Ni enye upole na kusadiki.

Ni enye kukuwa katika Mungu.

Ni kuwa kama Yesu.

Unyenyekevu wapendeza mbele za Mungu. Mtu mnyenyekevu na anayemwogopa Mungu hung’aa machoni pa Mungu. Unyenyekevu ni kutaka kumfurahisha Mungu na kutaka kutembea katika njia zake. Kujishusha na kutojifikiria kuwa bora kuliko wengine, kujiona chini ya wengine na kutowahukumu walio karibu nawe. Mimi pekee ndiye nafaa kuhukumu. Simaanishi ujifadhaishe ila uziheshimu hisia za wenzako. Na wanapoanguka, usiwadharau kimoyomoyo bali uwahurumie maanake hata wewe pia waweza kuanguka kwenye dhambi mbele ya Mungu aliye Mtakatifu.

Hivi ndivyo inavyokuwa mtu aki nyenyekea. Wanakuwa na ushuhuda wa kupendeza. Wanang’aa katika ufalme wangu, machoni mwangu. Nawapa sikio langu. Wanaponililia nawasikiza. Naweza kuwatendea lolote hata liwe gumu kiasi gani. Nitafanya lote liwezekanalo kwa ajili ya watumishi wangu wanyenyekeao. Je binti yangu, unayaelewa haya? Watumishi wangu wanyenyekevu wanajitolea kwangu.

Wanaelewa kuwa hawawezi kutenda lolote bila mimi. Kila mara wananitafuta kwa kila jambo jinsi mtoto amtafutavyo mzazi. Huyu ndiye mtumishi wangu mnyenyekevu. Hawana hiari yao. Wananiamini mimi katika mienendo yao ya kila siku. Wananitafuta ili wapate majibu yao kutoka kwangu. Huniamini kwa moyo wote nami huwajibu. Nawapa yaliyo mema maana wananitegemea kwa mambo yao yote. Ni wanyenyekevu na watukufu machoni mwangu. Wana uzuri mpole. Sio kama watu wa dunia.

Wanajitokeza kutoka kwa umati wa watu. Uzuri wao ni wa Kimungu na wa mbinguni. Hivi ndivyo mbinguni kulivyo – kumejaa watu waliosalama kwa Mungu wao kwa sababu nakutana na mahitaji yao yote.

Hawana haja ya kuwa wafidhuli na wenye kiburi. Mahitaji yao yote yatimizika kupitia kwangu. Wanaridhika, wananitumikia kwa hiari yao, na wanafurahia kuwatumikia wengine kuwa maana natosheleza mahitaji yao kila wakati. Hakuna yule anayepigania kuonekana kuliko wengine mbinguni. Kila mtu ameridhika. Mbinguni ni

1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 ... 17
Go to page:

Free ebook «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) by Susan Davis (ebook reader browser .TXT) 📖» - read online now

Comments (0)

There are no comments yet. You can be the first!
Add a comment