Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) by Susan Davis (ebook reader browser .TXT) 📖
- Author: Susan Davis
Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) by Susan Davis (ebook reader browser .TXT) 📖». Author Susan Davis
Natuanze, Binti yangu. Wanangu, Nataka kuwazungumzia kuhusu mada mpya.
Hivi karibuni, wanangu, nitafika na kuliondoa kanisa langu. Ni wachache sana ambao wa tayari… waningojea… wananitazamia.
Hili ni jambo zito, kweli. Ni wanangu wachache sana wanaonisikiza. Ni wachache sana wanaoyatilia maneno yangu maanani. Wengi hawasomi kitabu changu wala kuyatenda maneno yangu yaliyomo kitabuni humu. Hawazifuati sheria ambazo nimewapa. Wengi wanatenda wapendalo, bila kujali ninavyofikiria.
Wako nje ya mapenzi yangu kabisa, na wanatenda kulingana na hiari na mapenzi yao wenyewe.Mnapoenda mbali na mapenzi yangu, mnanipinga. Hili ni jambo la kuhuzunisha na wengi hawaamini neno langu na wameamua kuifuata dunia, badala ya kunifuata.
Wana, dunia ina uadui nami. Hamwezi kuwa nami, na dunia pamoja.
Yakobo 4:4. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.
Inamaanisha nini kuwa mmoja wa dunia? Ina maanisha kugeukia dunia ili dunia ikupe majibu yote uyatakayo: kufuata dunia kwa usalama wako, ukidhani kuwa dunia ina majibu yote. Huu ni usalama wa uongo – kutazamia majibu kutoka kwa binadamu. Binadamu asiyejua cho chote kuhusu yajayo. Ni mimi tu MUNGU nijuaye yajayo. Dunia inatafuta majibu kutoka kwa binadamu na mapepo mabaya. Mfumo wa dunia ni mfumo wa adui wangu. Anawataka wanangu wapotezwe na kila aina ya vitu ili wasinitafute niwape majibu. Kwa hivyo hawanitafuti ili kunijua kwa undani na kuwa na uhusiano wa karibu nami. Hii ni hatari sana wanangu.
Zaburi 20:7. Hawa wanataja magari na hawa farasi, Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.
Anawataka muwe mbali nami ili awanase na kuwaangamiza. Atatumia mbinu zote ili awanase. Atatumia huduma zenu, familia zenu, pesa na mali, burudani, na cho chote kile awezacho ili awapoteze. Hii ndiyo mbinu yake ya kuwafanya mniache na kuwa mbali nami.
Hii ndiyo mipango yake yakuwaangamiza na amefaulu kwa wengi wenu. Ni wachache sana wanaonifuata kwa karibu. Hili ndilo kanisa langu kamili. Hawa ndio wafuasi wangu kamili ambao wamejitolea kunifuata kikamilifu.
Mbona mnasisitiza kufuata dunia hali mimi ndiye nuru ya ukweli? Mimi ni uzima wa milele. Nawapa uhai, nawalinda. Mimi ndimi niyalindayo maisha yenu. Mimi ndiye niwapao uhai na kuuchukua tena ….hakuna mwingine.
Ayubu 12:10. Ambaye nafsi ya kila kilicho hai i mkononi mwake, na pumzi zao wanadamu wote.
Mbona mnashikilia kutonijali na kuwafuata wapenzi wengine? Wapenzi wasio na cho chote? Mwajichimbia shimo ninyi wenyewe….shimo ambalo hamtaweza kutoka ndani yalo.
Njooni kwangu. Tubuni na kuniachia maisha yenu. Ni mimi tu niliye na majibu. Ni mimi tu niwezaye kuwatendea yaliyo haki. Ni mimi niliye na ufunguo wa ufalme. Dunia hii haina cho chote cha kuwapa. Ni mateso, masumbuko kisha kifo hivi karibuni na uharibifu ujao duniani.
Acheni kuyaweka matumaini yenu kwa dunia ambayo imekufa… imekufa kwa maana hainitambui kama BWANA na MKUU wao. Hakuna Serikali ambayo inanitambua duniani.
Viongozi wote duniani wanafuata imani zingine, badala ya kunifuata mimi ambaye ni BWANA na MUUMBA. Hii ni makuruhi na sitakubali yawe hivyo. Dunia hainiogopi na kwa hivyo, nitawafunza tena ili wanitambue kuwa MIMI ni nani. Nitawachukua wachache waniaminio mahali pa usalama ndipo dunia itanitambua kuwa mimi sio MUNGU wa kuwekwa pembeni. Hivi karibuni nitauondoa mkono wangu wa kinga na adui wangu ataanza kutenda kazi yake duniani ... yeye na Jeshi lake la mashetani. Utakuwa wakati wa huzuni kwa wakaazi wa ulimwengu huu.
Zaburi 111:10. Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, wote wafanyao hayo wana akili njema, sifa zake zakaa milele.
Nifanye nini ili niweze kuwaelezea ukweli huu? Mniamini? Yote yameandikwa kitabuni mwangu, bali ni wachache sana wanaotaka kuujua ukweli. Mnakimbia huko na huko mkitafuta maarifa na busara, bali hamji kwa UKWELI.
Danieli 12:4. Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukatie muhuri kitabu hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka. Ni saa ya huzuni kwa wanadamu: watu wanaokimbiza dunia bali hawatamani kuwa na maarifa yatokayo kwa MUUMBA, wao. Huu ni wakati wa huzuni kwa binadamu. Matokeo ya kutonijali mimi MUNGU, ni wazi kabisa: uovu, magonjwa, uhalifu, kifo, uharibifu wa uchumi, vita na matetesi ya vita. Hii ndiyo shida binadamu wanayojiletea wakati wanamuacha MUNGU wao na kufuata dunia.
Wana, nirudieni. Hamjachelewa. Nitawatwaeni. Nawasubiri. Kimbieni mikononi mwangu. Njooni mnifuate.Tunaweza kuwa pamoja milele. Naweza kuwafanya muwe wangu. Na muishi maisha ya milele nami huko. Ndiyo wana, nifuateni, Muumba wenu au muifuate dunia bila mimi. Chaguo ni lenu. Nawajia watakaonichagua hivi karibuni. Wanipendao na wala sio wapenzi wa dunia. Chagueni kati yangu na dunia, kwa sababu ni sharti nije niwaokoe walio wangu. Wanaonichagua mimi badala ya kuchagua dunia. Mtafanyani?
Nasubiri kwa makini, bali si kwa muda mrefu. Hivi karibuni, ni sharti nimuondoe bi arusi nimpeleke mahali pa usalama. Huyu ni BWANA, NA MUUMBA WA dunia, YAHUSHUA.
SURA YA 22: UOVU WAJA KUINGAMIZA DUNIA
Natuanze tena. Wana, huyu ni BABA yenu anayezungumza. Nina maneno mengi yakuwapa leo.
Kuna dhoruba kuu ijayo ulimwenguni mwote. Inaitwa “uovu”. Yaja kuangamiza dunia na wakaazi wote.
Itakuja baada ya kumuondoa bi arusi wangu kwenda mahali pa usalama. Ataondoka kwanza. Hatashuhudia vitisho vijavyo. Baa lijalo nchini litawafanya wengi kuwa wazimu. Vitisho visivyo semekana vyaja. Utakuwa wakati wa vitisho tupu.
Waja watashtuka. Hakutakuwa wa kuaminika. Ni wakati wa vitisho ulioje.
Mpinga Kristo atatawala. Atatawala dunia nzima. Hakuna atakayeweza kumkomesha. Viongozi waliokuwapo walionyanyasa watu hawataweza kulinganishwa naye na tamaa yake ya damu. Hakuna wakufananishwa naye. Hakuna atakayeweza kujificha. Hakutakuwa na msaada wowote kwa yule atakayetaka kumuepuka. Kuepuka kutokana naye kutakuwa tu ni kifo. Huu utakuwa wakati mgumu katika historia ya binadamu.
Ufunuo 18:4-5. Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni na Mungu amekumbuka maovu yake.
Wana, amkeni na kuuona ukweli huu. Kisomeni kitabu changu. Yasomeni yatakayotukia. Kaeni chonjo. Jisalimisheni … njooni mikononi mwangu iwasubirio. Ni tayari kuwaokoa. Ni tayari kuwapokea, kuwabariki, na kuwaleta katika ufalme wangu mtukufu, kwenye upendo na uzuri wa milele. Nitawaleta kwenye karamu yangu ya ndoa ambapo tutaungana na kushiriki pendo letu milele na milele.
Hamuhitaji kuogopa siku za usoni. Hamuhitaji kuwaza juu ya mambo ya kesho. Mnachohitaji ni kujitolea kwangu. Jitoleeni kikamilifu. Nipeni yenu yote: maisha yenu, roho zenu, nafsi zenu, mioyo yenu, na mipango yenu yote. Nifanyeni niwe BWANA wenu. Nitawaongoza kwa usalama.
Ni wachache sana wajao. Ni wachache sana wanaotaka kushiriki kwenye wokovu wangu, nitakapo wapeleka wanangu kwa usalama kwenye mbingu zangu. Mtapokea miili mipya mitukufu. Itakuwa miili iliojaa nuru, nuru yangu ya mbinguni. Itanawiri, ya milele, isiobadilika na yenye utukufu. Wanangu, bi arusi wangu atakuwa mrembo sana.
Ndiyo, huku kubadilika kwa kanisa langu ku karibu. Hatakuwa alivyokuwa tena. Atakuwa na utukufu. Mabadiliko haya yatatendeka kwa kufumba na kufumbua macho kwa dakika moja, kanisa litabadilika tayari kwa BWANA ARUSI. Litakuwa tayari katika utakatifu na usafi.
1 Wakorintho 15:51-54. Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho, maana parapanda italia na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, mauti imemezwa kwa kushinda.
Atapendeza kwa mavazi yake yote. Namjia bi arusi wangu. Najua ananitazamia na kunitafuta. Imani yake ni imara. Yeye ndiye niliye mfia. Yeye ndiye aipokeayo zawadi yangu. Zawadi yangu ya wokovu nitoayo bure kwa binadamu. Ni wachache sana wanaoitikia zawadi hii na waifuatayo. Jambo hili lanihuzunisha sana; wana. Nilivuja damu nikafa kifo cha uchungu ili niwaokoe watu wote. Ni wachache sana wanaoutaka wokovu huu. Ni wachache sana wanaokubali wokovu huu na kujitolea kwangu.
Njooni wanangu, msiwe miongoni mwa wale watakaobaki na kupotea. Badilisheni nia zenu. Nitafuteni kwa mikono iliyo wazi. Kimbilieni mikononi mwangu, inayowangoja.
Saa hii inaisha haraka. Mu karibu kuuona mwanzo wa uovu na dhiki kuu. Amkeni. Zijazeni taa zenu na mafuta. Zikiwa bila mafuta hamtaweza kuja nami.
Mtakatifu Mathayo 25:4. Bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao.
Njooni mumpokee Roho wangu Mtakatifu kikamilifu. Atawawezesha kuwa na uhusiano wa ndani nami. Kisha nitawaosha katika damu yangu na kuondoa madoa yote kwa nguo zenu na kuwaweka tayari kwa ufalme wangu. Hivi ndivyo mtakavyokuwa bila ila wala kunyanzi lolote. Bi arusi wangu mrembo.
Waefeso 5:25-27. Enyi waume, wapendeni wake zenu, jinsi Kristo alivyolipenda kanisa, akajitolea kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Nataka kuwaleta pahali hapa, pahali pa uhuru na uzima wa milele. Njooni tu kwangu na mjitolee nami nitaanza kuwaweka tayari. Wakati unaisha. Amueni. Mwabaki au mwaja nami kwenye uhuru na usalama? Sasa wana, amueni. Nawataka muwe tayari, tayari kweli. Upendo wangu wawasubiri. Ni mimi mfalme wenu YAHUSHUA.
SURA YA 23: SAA SITA YA USIKU INAKARIBIA
Natuanze tena. Wana, huyu ni Bwana wenu anayezungumza nanyi. Nina maneno mengi ninayotaka kuwaambia.
Saa imefika, wanangu. Mnachelewa – saa inayoyoma. Saa sita za usiku zi karibu kutimia. Ni dakika mbili tu zimesalia.
Hii inamaanisha muna wakati mfupi sana wa kujitayarisha namaanisha kuitayarisha mioyo yenu na kuwa tayari. Ni saa ambayo kurudi kwangu kunakaribia sana. Kurudi kwangu ni kwa kumvuta bi arusi wangu nimuweke huru kutokana na ukaidi na gadhabu zitakazofuata. Hataathiriwa na yale yajayo. Bi arusi wangu ni mrembo na ametayarishiwa MFALME wake, na Bwana arusi wa Kifalme. Macho yangu ya kwake. Urembo wake unanitia bumbwazi. Ananifurahisha na ung’aavu wake. Ni watu walio tayari kumpokea BWANA ARUSI wao.
Wimbo ulio Bora 4:9. Umenishangaza moyo, umbu langu, Bibi arusi, umenishangaza moyo, kwa mtupo mmoja wa macho yako, kwa mkufu mmoja wa shingo yako.
Wamejitayarisha, wameoshwa kwa damu yangu. Wameoshwa na neno langu. Wananitazamia kwa hamu. Kila siku wananitazamia.Wananitarajia na kuniangalia pekee. Tuna ushirikiano wa ndani nao. Tunafahamiana. Watu wangu wamejitolea maishani mwao na wameachana na tamaa za dunia. Wananitumainia mimi tu. Wanautafuta uso wangu na sauti yangu. Wanaifahamu sauti yangu. Nizungumzapo hao hunifuata. Wanikimbilia.
Yohana 15:19. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi niliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
Nawathamini. Nawaongoza nao wanifuata. Maisha yao yanaangaza nuru yangu duniani. Hao ni mfano wangu kwa ulimwengu, ulimwengu unaoisha.
Hivi karibuni nuru hii itaondolewa duniani, na giza tu ndilo litakalosalia. Vivuli vitaingia na kutawala. Giza litatanda ulimwenguni mwote… pembe zote nne za ulimwengu. Itakuwa siku ya huzuni kweli.
Hamfai kuwa hapa wakati huu wa huzuni. Mwaweza kunifuata kwa kujitolea. Nitawaleta kwangu, niwakinge na kuwaongoza mahali pa usalama, nitakapokuja kulitwaa kanisa langu, kanisa langu bora. Yu tayari na nitamkinga kutokana na wakati huo wa giza kuu lijalo duniani. Wana, wakati wangu wa kurudi umewadia. Wakati uliosalia ni mchache sana. Ni sharti mjitayarishe. Kuna wakati kidogo uliobaki. Msiuharibu, kwa kufuata vitu visivyo na maana duniani. Utumieni wakati huu kujitayarisha.
Nifuateni kwa moyo wote. Tubuni dhambi zenu. Ninataka kusikia toba itokayo kwa moyo uliyojaa simanzi. Moyo wa mtu humdanganya. Ni miye pekee nionayo yaliyo moyoni mwa mwanadamu. Naweza
Comments (0)