Religion
Read books online » Religion » Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) by Susan Davis (ebook reader browser .TXT) 📖

Book online «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) by Susan Davis (ebook reader browser .TXT) 📖». Author Susan Davis



1 ... 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17
Go to page:
wa milele. 

Ndiyo. Niliwafilia kifo cha uchungu kwa msalaba muovu. Ulikuwa uchungu kweli. Ndiyo, nilimpa BABA yangu maisha yangu baada ya masaa mengi ya mateso katika mikono ya watu waovu, wapotovu, wenye chuki ambao walikuwa wanafanya mapenzi ya baba yao, adui yangu. Hii ndiyo gharama niliyolipia uhai na maisha yenu. Je, sistahili muda wenu, mapenzi yenu na kushughulikiwa miye?

Zaburi 22:12-16. Mafahali wengi wamenizunguka, walio hodari wa Bashani waminisonga; Wananifumbulia vinywa vyao, kama simba apapuraye na kunguruma. Nimemwagika kama maji, mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, na kuyeyuka ndani ya mtima wangu. Nguvu zangu zimekauka kama gae, ulimi wangu waambatana na taya zangu. Unaniweka katika mavumbi ya mauti. Kwa maana mbwa wamenizunguka; kusanyiko la waovu wamenisonga; wamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote; wao wananitazama na kunikondolea macho. Wanagawanya nguo zangu na vazi langu wanalipigia kura.

Njooni kwangu. Nawaambia mje kwangu. Niacheni niwachukue mikononi mwangu, niwashike, niwapapase, kama wanangu. Mimi ni BABA yenu awapendaye. Hakuna upendo mkuu kuliko wangu. Hakuna huba kuu kuliko yangu. Msininyime upendo wenu. Njooni kwangu mkinyenyekea katika toba. Niacheni niwasafishe, muwe wasafi mbele yangu. Niacheni niijaze mioyo yenu na furaha na raha. Naweza. Nataka. Wakati ni huu. Msingojee wala kusita. Huu ndio wakati wa kurudi kwangu. Naja kuwaondoa. Niacheni niwajaze na ROHO wangu. Niwafanye wakamilifu ndani yangu. Wakati unaisha wana. Hivi karibuni hakutakuwa na wakati tena uliosalia. Kwa hivyo, msidharau toleo hili la wokovu wangu pamoja na damu niliyoimwaga ili mpate ukombozi na kuwa wakamilifu milele.

Mathayo Mtakatifu 25:46. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

Natamani kuwa na uhusiano wa karibu na wa ndani nanyi. Ni wenu mkiniuliza. Nitawapa. Natamani kuwa na uhusiano wa karibu nanyi. Hamu yangu ni kuwa nanyi wakati wote kwa undani. Mkija kwangu kwa njia hii, hata nami pia nitakuja kwenu. Neno langu linaonyesha kuwa nataka kuwa na uhusiano wa ndani nanyi. Nawataka mnitafute mahali patulivu ambapo tunaweza kushiriki pamoja. Wanangu, mahali hapa ndipo ninapoweza kuwapa mafunzo namna ninavyotaka muishi maisha yenu. Mkinijia na kuwa na uhusiano wa ndani nami nitawaonyesha mipango yangu niliyo nayo juu yenu, na jinsi ninavyotaka muishi maisha yenu. Ila kwanza, lazima muwe kwenye mapenzi yangu, na kuwa kwa mapenzi yangu, ni sharti myatoe maisha yenu kwangu. Maisha yenu yote. Msiache cho chote. Myafanye maisha yenu yawe yangu. Myatoe kote kote. Muache mambo mengine yote pamoja na dunia. Nawataka muache mambo yote ya dunia na muwe tayari kunifuata po pote niwapelekapo. Watu wengi hawataki kufanya hivi. Wengi wamekwamilia vitu wasivyotaka kuviachilia. Wanangu, ni vitu gani vinawatenganisha nami? Ni kazi zenu? Ni mali? Ni huduma? Ni wana wenu? Ni nini hasa kinachowatenganisha nami? Ni kitu gani kinachowachangamsha kuniliko?

Mathayo Mtakatifu 10:37-39. Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi hanistahili. Wala mtu asiyechukua msalaba wake akanifuata, hanistahili. Mwenye kuiona nafsi yake ataipoteza; naye mwenye kuipoteza nafsi yake kwa ajili yangu ataiona.

Wana, msiponiweka wa kwanza, mtapoteza vyote vile vinavyowachangamsha na mimi pia mtanipoteza. Haya ni maneno yenye uzito lakini sina budi kuyasema. Nataka myasikie na kuangalia mliko ndani yangu. Mimi ni wa kwanza au wa mwisho maishani mwenu? Wanangu, pimeni nafasi zenu kwangu. Ni nafasi gani ninayoshikilia maishani mwenu? Wana, simameni karibu nami – natamani kuwaweka karibu moyoni mwangu. Saa ya kurudi kwangu yaja. Sitaki mbaki nyuma kwa mateso. Njooni na mtanipata. Kila wakati ni karibu nikiwasubiria mnifuate. Upendo wangu nu mkuu! Msikose kuufurahia upendo huu milele.

Huyu ni BWANA ARUSI WENU WA KIFAHARI YAHUSHUA

 

SURA YA 30: BI ARUSI WANGU APENDEZA KWA NJIA ZAKE ZOTE

Ndiyo binti, tuanze tena. Wanangu, ni mimi BWANA wenu. Nawasalimu katika jina la BABA YANGU ambaye ni BABA YENU pia. Wana, saa yangu ya kushuka chini ili kumtwaa bi arusi imefika. Apendeza kwa njia zake zote. Nafurahia kumwita wangu. Mpendwa wangu. Nitamchukua mikononi mwangu hivi karibuni. Atakuwa nami milele. Tutakuwa kama nyota, mimi naye. Upendo wetu hautakuwa na kikomo. Amani nimleteayo itadumu milele. Yeye ni bi arusi wangu mwema. Ananitii na anazipenda njia zangu. Ni mpendwa wangu naye hunifuata. Anatembea kwenye njia nyembamba. Anitazamia. Njia zake zapendeza. Yeye ndiye nuru ya mwisho iliosalia duniani. Anaonyesha dunia njia zangu. Dunia inaniona kupitia kwake. Anaonyesha yangu kwa ulimwengu. Njia zake ni za unyenyekevu na ana imani kama ya mtoto. Hii ni jinsi ya watu walio mbinguni. Saa ya kumtoa duniani ina karibia. Namchukua awe wangu. Namweka mahali pa usalama. Hivi karibuni atakuja nami mahali palipo salama ili asikumbane na mambo yajayo. Saa hii yaja, msiwe na tashwishi.

Mathayo Mtakatifu 18:3. Akasema, Amin nawaambia, msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

Nawataka mjiandae na kuwa tayari jinsi bi arusi wangu alivyojiandaa. Amejitayarisha kwa kujisafisha katika damu yangu. Amejisafisha na hana doa wala kunyazi lolote. Yu tayari kuja katika mbingu zangu, kuwa pamoja nami na kufuarahia kuwepo kwangu.

Waefeso 5:26-27. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake ili maksudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Ni tayari anijie mawinguni, aje juu. Hii ni siri. Siri kubwa mno, kwa maana atabadilika. Atafanywa awe nilivyo na mwili mpya mtukufu. 

Mwili wake utabadiliki: usio na dosari, usioangamia, ulio na nuru ya milele, NURU YANGU. Atang’aa mbinguni. Atakuwa na utukufu na kung’aa kwa sababu atakuwa jinsi nilivyo. Mwili huu hautokufa wala kujua kifo. Ni chemichemi ya ujana wa milele. Ni mwili usio na mipaka. Wanangu wataifurahia miili yao mipya. Hawatakuwa na uchungu tena. Miili hii itakuwa ikibadilika kulingana na mazingira. Watasafiri mbinguni bila shida. Miili hii itaweza kutembea au kupaa. Watafanya ifanyayo miili ya binadamu na mengine mengi zaidi. Ni miili ya nuru. Miili hii haitakuwa na kizuizi cho chote kama miili ya binadamu ilivyo. Wanangu watakula na kufurahia chakula kama wafanyavyo sasa. Yote kuhusu miili hii mitukufu itawabumbwaza wanaoipokea. Yote yatabadilika kwa pumzi, kwa dakika moja. Wanangu watabadilika kwa dakika. Itawafanyikia haraka sana. Watashangazwa sana, haya ni badiliko ya milele. Jicho halijaona wala sikio kusikia kile ambacho nimewaandalia wanangu. Wanangu waaminifu.

1 Wakorintho 15:51-54. Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutoharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutoharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapa ndipo litakapokuwa lile neno liloandikwa, mauti imemezwa kwa kushinda.

Geukeni na kunitazama mimi. Msikose tukio hili na utukufu huu, nirudipo kumchukua bi arusi wangu. Tukio hili laja wana, jiandaeni – fanyeni maandalizi muwe macho, mnifuate. Ni wachache sana wanaonitazamia. Wengi wamenaswa na dunia. Dunia inaonekana tulivu na sawa lakini ni uongo. Dunia inahadaa. Ina uovu tele na mnaukumbatia. Inakwama kwenye uongo na kuufanya kama ukweli —hakuna ukweli duniani. Dunia inakuhadaa kuwa mambo ni shwari na hali si hivyo. Hivi karibuni mtayaelewa haya yote. Jitayarisheni. Sitasubiri muda mrefu. Kuja kwangu ku mlangoni. Nasimama mlangoni nikibisha. Niacheni niingie mioyoni mwenu. Saa inapita. Muda unakwisha. Ondokeni kwa ulegevu na mpige magoti. Tubuni dhambi zenu. Nipeni maisha yenu nami nitawasafisha na kuwafanya muwe tayari. Natamani kufanya hivi. Jitengeni na dunia. Jitengeni na dunia, ondokeni. Dunia ni kifo. Haitaendelea bila mimi. Maangamizi yake yametokana na kunipa mimi kisogo na kuendea mambo maovu.

1 Wathesalonike 5:23. Mungu wa amani Mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili bila lawama wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.

La wana, ni sharti muamue. Mtaenda na dunia au mtakuja nami? Ni uamuzi wenu. Siwezi kuwaamulia. Niwezalo ni kuwaomba tu mje kwangu. Nawataka muwe upande wangu milele. Natamani muwe nami mbinguni. Ila ni uamuzi wenu. Mjitolee kwangu ama mbaki nyuma. Naungojea uamuzi wenu. Upendo wangu ni mtulivu. Mimi ni MUNGU asiyedanganya. Nijieni kabla ya muda kwisha.

Ni MIMI MKUU YAHUSHUA.

 

 

SURA YA 31: NI WACHACHE SANA WANAONIABUDU NA KUTUBU KWANGU

Haya, natuanze (Februari 28, 2012). Wanangu niwahusuduo, saa ya kurudi kwangu inawadia. Ni sharti mjiandae. Ni sharti mjitayarishe. Jifunikeni kwa damu yangu. Dunia inaisha. Inafikia kikomo. Inabadilika. Ina uozo wa maadili. Inanuka kwa uovu mtupu. Inanigeuka mimi MUNGU wake. Ni wachache sana wanifuatao kwa kiwango nihitajicho kutoka kwao. Ni wachache sana wajitupao miguuni pangu kuniabudu na kutubu kwangu. Ni wachache sana watakao kunifuata ko kote kule nitakako waende bila kusita.

Marko Mtakatifu 8:34. Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.

Wengi wameshikwa duniani wakifuata vitu vya duniani. Hamjui kuwa dunia hii ina uadui nami? Sitaistahamili dunia hii tena. Sitairuhusu dunia iendelee inavyoendelea. Hivi karibuni nitamwondoa bi arusi wangu na kuwavuta wanangu niwapeleke kwa usalama. Bi arusi wangu apendeza na ni tayari kumpokea kwa nyumba niliyomwandalia juu mbinguni. Hakika tukio hili li karibu kutendeka. Wanangu mwahitaji kuelewa mambo haya. Yafaa mwelewe ukweli huu. Wengi wanasinzia, wamelala fofofo. Wanaenda mbali nami. Wanaanguka mikononi mwa adui na hivi karibuni kama ndege ambaye anashikwa mtegoni mwa wawindaji watashikwa.

Zaburi 124:7. Nafsi yetu imeokoka kama ndege katika mtego wa wawindaji.

Amkeni wanangu, muone ukweli. Amkeni na mtizame, naja! Amkeni kabla hamjapatwa na kuniacha kabisa. Sasa yangu ya kurudi imefika na wengi wangali wanalala –wamelala fofofo. Huu si wakati wa kupatikana mkiwa hamjajitayarisha! Amkeni! Hivi karibuni adui atawaweka mahali awatakapo ninyi nyote muwe, msiponijia na kujitolea kwangu kabisa. Huu ni wakati wakumtii MUNGUwenu kabisa. Mimi ni MUNGU mvumilivu, ila uvumilivu wangu karibuni utakwisha. Sitastahamili dunia hii ambayo yafa. Yafa kwa sababu inamkataa MUNGU aliyeiumba. Kila pembe ya dunia imenikataa. Nimekataliwa kote. Dunia sasa inakumbatia uovu. Inakumbatia uovu, inalala na uovu, inaamka kutenda uovu na kulala na uovu. Bi arusi wangu pekee ndiye anifuataye. Yeye tu ndiye mwaminifu. Yeye tu ndiye aliye na mikono misafi. Yeye tu pekee ndiye anayenifuata na amejitenga na dunia. Ni yeye tu pekee ambaye hajachafua nguo zake kwa kushiriki kwa mambo ya dunia. Yeye ni nuru yangu katika dunia iliyojaa giza. Anang’aa gizani. Nuru yake inaweka kimulimuli kwa dunia iliyojaa giza tele, dunia ambayo inajaa giza kila siku. Hivi karibuni nuru hii itazimika kwa maana ni sharti nimuondoe nimpeleke mahali palipo salama. Kisha dunia itaendelea kuwa na giza bila matumaini yo yote. Huu ni wakati mgumu wanangu. Ni sharti mje kwa nuru yangu wakati mungali na nafasi. Wakati uliobaki ni mdogo mno. Saa i karibu kwisha. Mshale wa dakika unakaribia sa sita za usiku. Msiyapuuze maneno haya ninayowaambia. Ni kwa manufaa yenu: Kuwaepusha na madhara. Kuwaepusha na yajao.

Yohana Mtakatifu 8:12. Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

Wanangu, nawapenda jinsi baba mpendwa anavyowapenda wanawe. Nawataka mje mikononi mwangu ambamo mtakuwa salama. Ni kupitia kwangu tu ndipo mtapata usalama. Kuwa ndani yangu na kupitia kwangu ndiko

1 ... 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17
Go to page:

Free ebook «Marriage Supper of the Lamb (Swahili version) by Susan Davis (ebook reader browser .TXT) 📖» - read online now

Comments (0)

There are no comments yet. You can be the first!
Add a comment